Tuesday, May 22, 2012

FLAVIANA MATATA AZULU KABURI LA MAMA YAKE MZAZI KUKUMBUKA AJALI YA MELI YA MV BUKOBA

Mwanamitindo, Flaviana Matata (wa pili kulia) akiomba dua katika kaburi la mama yake Mzazi maeneo ya Igoma mkoani Mwanza katika siku ya kukumbuka ajali ya MV Bukoba iliyoua watu takribani 1000  Mei 21, 1996.  Flaviana mbali na kukumbuka waliofariki katika ajali hiyo akiwamo mama yake mzazi pia alikabidhi msaada wa vifaa vya kuokolea maisha  kwa Shirika la Kiserikali la Usafiri wa Maji Mwanza.
 Mwanamitindo wa kimataifa wa mitindo Tanzania, Flaviana Matata akikabdhi moja ya kifaa cha kuokolea maisha katika vyombo vya  usafiri wa majini katika Ziwa Victoria kwa Elias Makori aliyemwakilisha  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  jana. Flaviana alikabidhi vifaa hivyo kwa Shirika la Kiserikali la Usafiri wa Maji Mwanza (Mwanza MerineCompany Limited)  ikiwa moja ya kuadhimisha siku ya hudhuni ya ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea Mei 21 mwaka 1996 na kuuwa watu zaidi ya 1000 akiwemo mama yake mzazi.

No comments:

Post a Comment