Showing posts with label Zimbabwe. Show all posts
Showing posts with label Zimbabwe. Show all posts

Sunday, December 7, 2008


Hivi ndivyo ilivyo nchini Zimbabwe kwa sasa. Hali inazidi kuwa ngumu lakini bwana Mugabe hasikii wala haoni. Hivi kama kweli mwendo ni kwa mkokoteni, hawa wagonjwa wa kipindupindu watapona kweli? Mugabe sasa inatosha...ONDOKA!!

Sunday, November 30, 2008


Kama bwana Mugabe ameshindwa kuwapatia wananchi wake unafuu wa kupata hata maji, hivi ni nini kinamfanya afikirie kwamba anahitajika tena? Kwa sasa Wazimbabwe wanakufa kwa kipindupindu na njaa, lakini mheshimiwa bado anadhani yeye na uongozi wake sio tatizo ila ni wapinzani. Hawa ndio viongozi wetu Afrika! Je kweli tutafika?