Saturday, February 27, 2010

Mwanamziki mkongwe HAMISI KITAMBI amefariki dunia leo 26 February 2010 Dar-es-salaam,

MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI saa 7.00 mchana 27-02-2010 MAGOMENI,Ifunda ,jirani na shule ya Mzimuni, Jijini  Dar-es-salaam.



Mwanamziki mkongwe wa dansi Bw.Hamisi Kitambi,amefariki dunia siku Ijumaa alfajiri ya tarehe 26/02/2010  katika Hospatali ya Muhimbili.

Marehemu aliwahi kupigia bendi za Msondo Ngoma ,kabla ya kupata maumivu ya mguu yaliotokana katika hajali alipokuwa safarini na bendi ya msondo ngoma . Marehemu pia alikuwa mwanamziki nyota enzi za Tabora jazz, ambako alipigia bendi ya Tabora kabla ya kuhamia Juwata Jazz sasa Msondo Music band.

Kwa taarifa zaidi tafadhali mnaweza kuwasiliana kwa simu na familia ya marehemu kwa simu namba 0713 802370 Almasi Kassanga, au Bi. Mwamini Kitambi simu namba 0712 217740



Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi

Amin

No comments:

Post a Comment