Wednesday, June 23, 2010

BUTI JIWE KUKAMUA MJINI EMMEN,HOLLAND
Jumamosi 26-06-2010
Mwanamziki Buti jiwe aka Henry Galinoma,Jr. mwenye maskani yake nchini Uholanzi anatarajiwa kutingisha jukwaa la onyesho kubwa la Midzomerhout Festival,mjini Emmen, huko Holand.  Mwanamziki huyo wa mziki wa dansi wa afrika mashariki amechaguliwa kuwa ndiye mwanamziki pekee wa kiafrika nchini Uholanzi kuwakilisha katika onesho hilo, ambapo pia atawaongoza jukwaani wanamziki watakao kwenda na mwavuli wa jina la "Africa Breezze".  Mwanamziki Buti Jiwe ameachia hewani album iliyobeba jina la "Samahani" ambayo inatamba katika vituo vingi vya redio ndani na nje ya Tanzania, hata hivyo Buti Jiwe ameahidi kuachia Remex ya album hiyo, kabla ya kumalizika mwaka 2010, hili kuhakikisha washabiki na wadau wa mziki wanapata mdundo wenye kuleta "Raha" katika burudani ya mziki.Buti Jiwe amewaomba wadau na washabiki wa mziki walio ndani na nje ya Bongo kukaa mkao wa kula!! CD za Buti Jiwe zinahitaji pia msambazaji mzalendo, atakaye sambaza CDs katika nchi za afrika mashariki.