Tuesday, June 22, 2010

LEO KATIKA KUKUMBUKA SIKU YANGU NILIYOZALIWA,  NINGEPENDA WATANZANIA WOTE  NJE NA NDANI YA TANZANIA TUWAOMBEE VIONGOZI WETU WAPATE HEKIMA NA BUSARA YA  KUTUONGOZA  ILI NCHI YETU INEEMEKE KWA MAZURI.

TUWAOMBEE WAACHE "UBINAFSI",  KWANI NDIO CHANZO CHA MATATIZO YETU MENGI NCHINI.  NA TUWAOMBE WALIOSHINDWA UONGOZI WAACHIE!!  WAKO WATANZANIA WENGI WENYE UWEZO MKUBWA WA KUWEZA KUIONGOZA  NCHI, TENA WENYE MTAZAMO NA UPEO WA HALI YA JUU.

WATANZANIA WALIPA KODI NAWAOMBA MUONYESHE UCHUNGU NA PESA YENU KWA KUWA WADADISI  NA NI NINI MNAFAIDIKA NA ULIPAJI WA KODI HIYO.

WATANZANIA MLIO NDANI NA NJE TUSIKUBALI TENA KUENDELEA KUWA "WANANCHI" BALI TUWE "WENYENCHI" KWA KUSHIRIKI KWENYE MAAMUZI MUHIMU NCHINI MWETU.  TUWACHE KUTOA MALALAMIKO WAKATI SISI WENYEWE NDIYO TULIOWACHAGUA VIONGOZI WABOVU. UCHAGUZI UKO NJIANI NA TUNA HAKI YA KUTOMPA KURA ZETU YE YOTE AMBAE HAFAI.

TANZANIA TUNAWEZA KUPIGA HATUA KUBWA YA MAENDELEO KWA WATU WETU NA NCHI YETU.  UONGOZI SIO "AWAMU"  BALI NI DHAMANA.

NAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ANIJALIE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU NA NAMSHUKURU KWA HAPA ALIPOKWISHA NIFIKISHA!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!