Siasa ni
kitu kizuri sana hasa kikitumiwa kwa malengo yanayotakiwa na hasa
katiika kuleta maendeleo, daima wanasiasa huwa na malumbano na
kuoneshana chuki wanapokuwa katika mambo mengi ya kutafuta maendeleo ya
wananchi wao na taifa kwa ujumla. Juzi Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe alizua hoja ya kutafuta saini 70 za kumuondoa Waziri Mkuu
madarakani zoezi ambalo linadaiwa kukamilika hadi sasa.
Mtu mwingine
anaweza sema kwa kauli ile huenda sasa Pinda na Zitto wakawa ni maadui
lakini hakika ile ni siasa na mambo ya siasa ni siasa na urafiki na
ujamaa wao upo pale pale kama hivi wanavyoonekana katika picha hii
iliyopigwa leo mjini Dodoma nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma
Pichani za
juu zinamuonesha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge,
John Mnyika wa Ubungo
(kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini na Hamad Rashid wa Wawi,
kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012.
lakini huku
mtaani washabiki wa siasa hizo saa ingine wanaumizana, kuchukiana na
kushindwa kusikilizana kwa namna yeyote ile.
|
No comments:
Post a Comment