Kesi ya uchaguzi ya kupinga kutangazwa kwa ndg Aeshi Hiraly CCM kuwa
mbunge wa Sumbawanga mjini leo mashahidi wa pande zote mbili
wamehitimisha kutoa ushahidi wao mbele ya jaji wa mahakama kuu mh
Jaji`Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla “J.4”(Judge incharge mahakama kuu
Mbeya). Kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama kuu mjini Sumbawanga,
ambapo hoja za msingi zilizokuwa zikisikilizwa ni, moja, mchakato mzima
wa uchaguzi kugubikwa na rushwa iliokuwa ukitolewa na mgombea wa CCM na
pili ni uchakachuzi wa matokeo uliopelekea kutangazwa kwa bw Aeshi.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na bw Noberth Yamsebo aliyekuwa mgombea
ubunge kwa tiketi ya CHADEMA (mlalamikaji) anayetetewa na wakili mmoja
toka mbeya na upande wa washitakiwa unatetewa na mawakili wanne. Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa rasmi tangu tarehe 27/03/2012 na leo tarehe
14/03/2012 ndio mashahidi wote wamemaliza kutoa ushahidi wao, upande wa
mlalamikaji ulikuwa na mashahidi 25 na upande washitakiwa ulikuwa na
mashahidi wanne tu ambao wawili kati yao “ bw Vitusi Silago mchambuzi wa
mifumo manispaa ya Sumbawanga na bi Silvia Siriwa aliyekuwa mkurugenzi
wa manispaa na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la sumbawanga mjini”
(kwa sasa yuko halmashauri ya wilaya ya Ileje kama mkurugenzi) ndo
wamefunga pazia la mashahidi. Vielelezo mbalimbali vilitolewa upande wa
mlalamikaji na mashahidi kama ushahidi kuihakikishia mahakama kutilia
manani hoja za msingi za kesi hii, moja kati ya vielelezo hivyo ni fomu
mbalimbali zilizotumika kujaza, kujumlishia na kutangazia matokeo ya
ubunge ambazo zilitumiwa kuchakachulia matokeo, mashahidi upande wa
mlalamikaji walitoa ushahidi wao dhidi ya mgombea wa CCM ukiwepo wa
kununuliwa pombe, kununuliwa baiskeli, kupewa fedha cash, ununuzi wa
shahada za kupigia kura, ununuzi wa vinanda “keyboard” kwa ajili ya
kwaya za makanisa mbalimbali na kuwa vyote hivyo vilitolewa kwa
mashariti ya kumpigia kura mgombea wa CCM bw Aeshi |
No comments:
Post a Comment