Wednesday, May 2, 2012

*BREAKING NEEEWZ! MAKONGORO MAHANGA ASHINDA KESI YA UCHAGUZI JIMBO LA SEGEREA DHIDI YA MPENDAZOE .

Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakirindima kwa shangwe na furaha huku wakiimba na kucheza katakati ya barabara ya Kivukoni wakitoka mahakamani hapo baada ya hukumu hiyo.

Shangwe, nderemo na vifijo, vimesikika nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam muda mchache uliopita baada ya kutolewa hukumu ya Kesi ya uchaguzi wa 2010 katika Mbunge wa Jimbo la Segerea Makongoro Mahanga wa CCM na Mpendazoe wa Chadema. Baada ya hukumu hiyo mashabiki wa Mbunge huyo na wafuasi wa CCM waliofika kusikiliza hukumu hiyo, walilipuka kwa makelele ya kushangilia mahakamani hapo. Pichani Mahanga akiwa amezungukwa na Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati akitoka Mahakamani hapo muda mchache uliopita.

Wafuasi wa Chadema Baada ya Hukumu Kutolewa.\ Mahakamani Hapo.

Nje ya Mahakama Wana Chadema.....

No comments:

Post a Comment