Upi ? Msimamo wa viongozi wa nchi Afrika kuhusu
Libya?
Je ? wanamtambua kiongozi halali wa Libya?
Vipi ? kiongozi wa waasi Mustafa Abdel-Jalil
anatambulika na Viongozi wetu?
Wakati viongozi wa nchi mbali mbali wamekutanika mjini
New York, kwa ajili ya mkutano wa umoja wa mataifa UN, katika mkusanyiko huo
wamo pia viongozi wetu kutoka nchi za kiafrika ambao pia ni wanachama wa
umoja wa Afrika AU, ambayo Libya pia ni
mwanachama wa AU,lakini utata unakuja nani kiongozi halali wa nchi hiyo Libya? Kanal Gaddaf au Mstafa Abdel-Jalil
ambaye nae yupo huko New York.
Swali lingine kubwa ambalo wengi wetu tunajiuliza je
?viongozi wa nchi za Afrika wanautambua uhalali wa Mstafa Abdel- Jalil ?kama
hawautambui je? watakubali kuwepo ukumbini na kumsikiliza otuba ya
kiongozi huyo aleyeingia madarakani kwa njia ya bunduki tena kwa kusaidiwa na
NATO? au watakuwepo
ukumbini kwa mithali za kiswahili kila moja na lwake?
yaani ya Ngoswe muachie Ngoswe! je? fadhila za Kanal Gaddaf na mchango wake
katika bara la Afrika ndio zitakua zimesauliwa.
Mengi tunajiuliza lakini siye wafrika tunategea sikio
uko UN kusikiliza msimamo wa viongozi wetu juu ya kauli ya pamoja kuhusu maslahi
ya bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment