Saturday, September 17, 2011

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
 
TAARIFA KWA UMMA

NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.

Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

MKOA
WILAYA ZAKE
MKOA ZINAKOTOKA
MAKAO MAKUU
1.
Geita
Geita
Mwanza
Geita
Nyang’hwale(Mpya)
Mwanza
Chato
Kagera
Bukombe
Shinyanga
Mpya/Mbogwe
Shinyanga
2.
Simiyu
Bariadi
Shinyanga
Bariadi
Itilima (Mpya)
Shinyanga
Maswa
Shinyanga
Meatu
Shinyanga
Busega (Mpya)
Mwanza
3.
Njombe
Njombe
Iringa
Njombe
Wanging’ombe(Mpya)
Iringa
Ludewa
Iringa
Makete
Iringa
4.
Katavi
Mpanda
Rukwa
Mpanda
Mlele(Mpya)
Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYA
WILAYA MAMA
MKOA
MAKAO MAKUU
1.
Buhigwe
Kasulu
Kigoma
Buhigwe
2.
Busega
Magu
Mwanza
Igalukilo
3.
Butiama
Musoma
Mara
Nyamisisi
4.
Chemba
Kondoa
Dodoma
Chemba
5.
Gairo
Kilosa
Morogoro
Gairo
6.
Ikungi
Singida
Singida
Ikungi
7.
Itilima
Bariadi
Shinyanga
Itilima
8.
Kakonko
Kibondo
Kigoma
Kakonko
9.
Kalambo
Sumbwanga
Rukwa
Kalambo
10.
Kaliua
Urambo
Tabora
Kalua
11.
Kyerwa
Karagwe
Kagera
Rubwera
12.
Mbogwe
Bukombe
Shinyanga
Mbogwe
13.
Mkalama
Iramba
Singida
Nduguti
14.
Mlele
Mpanda
Rukwa
Inyonga
15.
Momba
Mbozi
Mbeya
Ndalambo
16
Nyang’hwale
Geita
Mwanza
Nyang’hwale
17.
Nyasa
Mbinga
Ruvuma
Mbamba Bay
18.
Uvinza
Kigoma
Kigoma
Lugufu
19.
Wanging’ombe
Njombe
Iringa
Waging’ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

Fax- 026-2322116

 Imetolewa na: -

 Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


9 Septemba, 2011

No comments:

Post a Comment