CECILIA AWASHUKURU
WATANZANIA
Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu.
Mtoto Cecilia Edward ambaye
anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amewashukuru kwa
moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia kwa hali na mali mpaka
kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu anayotarajia kwenda kuyapata nchini
India.
Cecilia amesafiri kuelekea katika
hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New Delhi -India kwa matibabu, jumatatu
ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka huu.
Aidha walezi wa Sesilia familia ya
mzee Kambaliko inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo
kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya faraja
pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.
Kabla ya safari yake hiyo, hali ya
kiafya ya sesilia ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na
kukaa, tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo
lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya kuanza
safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
Mtoto huyu aliondoka hapa nchini
jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana na
daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja na mlezi mmoja
mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa na madaktari tayari kwa
uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.
Kipindi cha Mimi na Tanzania
kinapenda kuwashukuru Watanzania wote pamoja na makampuni mbalimbali
yaliyojitolea katika kumsaidia Sesilia kwa ajili ya matibabu. Shukrani za pekee
ziifikie hospitali ya regency hasa daktari Kanabar kwa uvumilivu na huduma nzuri
kwa Sesilia. Pia kwa mchango wao wa kulipia nauli ya kwenda nchini India kwa
Sesilia, mzazi na daktari ikiwa ni pamoja na matibabu ya awali anayoyapata hivi
sasa.
Watanzania, pamoja tumeweza tena.
Sesilia ni mmoja tu kati ya watoto milioni moja wanaosumbuliwa na tatizo hili,
hebu tujitolee kuwasaidia watoto hawa bila ya kuchoka, pia tusimsahau binti huyu
kwa maombi ili upasuaji anaotarajia kufanyiwa umalizike salama na kwa mapenzi
yake Mungu mtoto huyu arudie katika hali ya kawaida kama watoto
wengine.
Mungu mbariki
Sesilia.Amen!
No comments:
Post a Comment