"MJUE SENSEI RUMADHA FUNDI"
Wakati
tunaelekea katika shangwe za miaka 50 ya Uhuru, tunawaletea makala maalumu ya
matunda ya vijana walizozaliwa ndani ya miaka 50
ya uhuru,Tanzania pamoja na kuwa na watalaamu wa fani na taaluma mbali mbali
lakini tunao wataalammabingwa wachache sana katika
nyanza au fani ambazo ni adimu sana,watalaamu hao mojawapo ni mkufunzi
bingwa wa michezo ya KARATE NA YOGA ,Mtanzania
Sensei Rumadha Fundi,anayeishi kule Marekani aka nchi ya herufi tatu USA, Darubini yetu imemnasa na kama anavyoelezea:
Muktasari wa Sensei Rumadha Fundi
”Romi”(Sandan)
Naitwa Rumadha Fundi, “Sensei Romi”Mvuto wangu katika
sanaa ya Karate ulianza wakati nilikuwa mdogo mnamo miaka '70s pale
Kariakoo,jiji Dar, lakini asili ya kwetu ni Tabora. Kwa bahati nzuri, jirani
yetu pale mtaani(Aggrey/Congo) Dar-es-salaam ambako Sensei Bomani alikuwa
anakuja kuwafuata baadhi ya wanafunzi wake enzi hizo. Hapo ndio ulikuwa mwanzo
wangu wa kujua hasa kuhusu Goju Ryu Karate.
Mwaka '78 mwishoni nilipata fursa ya kutembelea “Hekalu
la Kujilinda” Zanaki Dojo Kan Shibu, nakuongea na Senpai Magoma Nyamuko Sarya.
Kipindi hicho Sensei Bomani alikuwa amekuja toka Marekani na kuja kuwafanyia
mitihani wa daraja la “Nidan”kina Senpai Magoma Nyamuko Sarya (Mwafunzi
kiongozi), Senpai Tola Sodoinde Malunga, Sensei Gamanya nk. Ndipo nilipoanza
shughuli za mafunzo kama”Teenager class”lilijulikana kama (Bomani
Brigade)
Baada ya mtiani wa mkanda wa kahawia
'81, kiongozi wetu (Senpai Magoma) aliondoka kwenda India na Phillippines
kusomea sanaa mbalimbali na Yoga , ndipo na mimi nikajiunga nae huko India na
baadae kwenda Sweden mnamo mwaka wa '85 katika shule ya Yoga”Internation school
of Intution Practice” au katika lugha ya Sanskrit ambayo ndio inatumiwa na Yoga
hujulikana kama “Prakshimata - Ananda Nilayam” huko, Gullringen, Vimmerby,
Sweden.
Hapo ndipo lipohitimu ualimu wa Yoga
baada ya kozi ya miaka miwili na kurudi tena Calcutta, India kwa Master mkuu wa
Yoga duniani na hatimae kupata ngazi ya juu katika mafunzo ya Yoga mnamo mwaka
wa '90 “Avadhuta”.
Vile vile nilipata fursa ya kwenda
Houston, Texas mwaka '88 na kuendelea na mafunzo ya Karate mtindo wa “Okinawa
Goju Ryu” chini ya uongozi wa Master Sensei Morio Higaona mwenye Dan 10,
kiongozi mkuu wa “International Okinawan Goju Ryu Karate -Do Federation” na
kupata fursa ya kupata daraja la kwanza '89 toka kwa Master Higaona huko
Tampico, Mexico chini ya uongozi wa Sensei Mario Falcone wa Mexico na Sensei
Ramon Veras wa Houston, Texas. Hawa ni moja ya walimu walio nisaidia kwa dhati
katika sanaa ya Karate. Ninapenda kutowa shukran nyingi kwa walimu wote ambao
waliweza kunifundisha sanaa hii sehemu zote zile nilizoweza kushiriki katika
fani hii kama vile, Master Morio Higaona, Master Teruo Chinen, Sensei kiongozi
wa Okinawa Goju Ryu, in Okinawa, Sensei Matsuda, na Sensei Muramatsu.Hao wote
ni viongozi wa ngazi za juu sana duania katika sanaa ya mtindo wa Goju.
Kwa sasa hivi nina daraja la tatu “Sandan”mkanda mweusi
kwa muda mrefu sasa. Kumbu kumbu yangu kubwa ni kuwa na ushirikiano mwema na
wanafunzi wengi wa zamani pale “Hekalu la Kujilinda” ambao sasa hivi bado wapo
mbele katika kusaidia vijana kama Sensei Maulid Pambwe, Rashid Almas, Mohamed
Murudker, Wilfred Melkia, Geofrey Sawayael “Shoo”, Mbezi, Metthew huko Mwanza,
Ndaukile,Edgar Kaliboti huko Sidney Australia, Salum Kitwana Khamisi huko UK.
Hata wale wote ambao nimewasahau popote pale duniani.
Pia, natoa shukran nyingi sana kwa mtu
muhimu sana katika maisha yangu ya kisaa ya Karate na Yoga ambaye ulikuwa ndio
mashine ya mafanikio yangu ngazi zote hizo, Senpai Magoma Nyamuko
Sarya(Mahadev/Mrnal) popote pale alipo nasema,”Shkran”.
Mipango ya uendelezaji sanaa hii kwa miaka ya mbele huko
Tanzania ni muhimu sana. Moja ya hiyo mipango ni siku moja kufungua chuo cha
sanaa ya kujilinda na kutumia nyezo za Karate”Kobudo” Kama vile “Sai, Tonfa,
Nunchaku,Bo, Shuri, “Three section Nunchaku” nk. Kwa ajili ya kufundisha
Tanzania. Ingawa sio leo wala kesho, bali ni moja ya mipango ya mbele huko
katika maisha nitaporudi Tanzania, nakuwashirikisha walimu wengine wenye uzoefu
mwingi katika kutumia nyenzo hizo.
Sensei
Rumadha fundi pia at facebook Romi Fundi
No comments:
Post a Comment