Friday, July 26, 2013

UBALOZI WA MAREKANI WAIPONGEZA TTCL KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA MAWASILIAN​O WAKATI WA UJIO NA UWEPO WA RAIS BARACK OBAMA



Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.

Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango wa TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani alipotembelea Nchini Tanzania.
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
*******
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa Marekani kwa huduma bora iliyotoa wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa nchini.

Akitoa shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora na za uhakika kutoka TTCL wakati wote wa ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza kuwa huduma walizozipata zimethibitishwa na taarifa kutoka ofisi inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi walizopita Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya kiwango cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

Akipokea salam hizo za shukrani kutoka kwa ujumbe huo wa Marekani, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura amesema, TTCL ilifanya kazi yake kwa uhakika na ina uwezo wa kuhimili mahitaji ya watanzania na Kimataifa pia.

Ameongeza kuwa TTCL inaendelea na juhudi za kujikita zaidi katika huduma ya data/ intanet na kuendelea kuboresha gharama ili kila mtanzania apate fursa ya kunufaika na mawasiliano ya simu pamoja na data.

Katika Shukurani zake Bw. Jeff Shrader alioa pia zawadi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura na kwa baadhi ya wawakilishi kutoa fani mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL kama ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment