Friday, July 26, 2013

POLISI 3,092 WAMEHITIMU MAFUNZO CCP MOSHI WANAKUJA MTAANI

Zaidi ya Askari Polisi wapya 3,092 wamehitimu mafunzo yao ya awali ya Polisi katika Chuo cha Polisi (CCP) kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro hii leo.

Polisi hao wapya ambao wanaingia mtaani nchi nzima wataingia mtaani wakati wowote kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao unakuwa madhubuti.

Mafunzo yao yamefungwa chuoni hapo na Waziri Mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa kushuhudia maonesho mbalimbali ya vitu walivyo jifunza jambo ambalo endapo kama watalitumia vyema basi litaleta chachu katika kukabiliana na uhalifu unao tikisa katika maeneo mbalimbali ya nchi pamoja na watu wasio tii sharia hadi washurutishwe. 
Maonesho ya Careti yakifanyika
Kareti hiyoo
Ukakamavu

No comments:

Post a Comment