Saturday, July 21, 2012

Taswira Mbalimbali za Viongozi Waandamizi wa Serikali,Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mabalozi Wakitoa Mkono Wa Pole Kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kufwatia Ajali ya Meli ya M.V Skagit iliyozama Karibu na Kisiwa Cha Chumbe

  Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Ali Abdulla Ali akiwa na Makatibu wake wakitoka nje ya Ukumbi wa Baraza hilo baada ya kuahirisha kwa siku moja kikao cha baraza la Wawaklilishi jana asubuhi. Hatua hiyo imekuja kufuatia msiba uliolikumba Taifa baada ya ajali ya Meli ya M.V Skagit iliyozama karibu na kisiwa cha Chumbe
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wabunge wa Muungano waliofika Zanzibar Kutoa mkono wa pole hapo katika ukumbi wa Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Mbweni kufuatia Ajali ya Meli ya M.V. Skagit. Ujumbe huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua baadhi ya majeruhi wa M.V Skagit waliolazwa katika Hospiotali Kuu ya Mnazi Mmoja wa tatu kushoto ni rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan Mwinyi
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema akitoa Taafifa ya uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo Ofiosini Vuga Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji baadhi ya Watalii na wageni waliokuwa wakija Zanzibar kwa Meli ya M.V. Skagit iliyopata ajali juzi mchana karibu na Kisiwa cha Chumbe. Kulia ya Balozi ni Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Mh. Hamad Masoud Hamad.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema akitoa Taafifa ya uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo Ofiosini Vuga Mjini Zanzibar.Picha na Saleh Masoud Mahmoud – Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

No comments:

Post a Comment