Kutoka kwa mwandishi wetu.
DAWA ZA KULEVYA ZAWATOA WATANZANIA.
Wimbi la Watanzania kuhusika ama kuhusishwa na biashara na matumizi ya dawa za kulevya,linazidi kuongezeka kuongezeka katika anga za kimataifa.
Katika kuongezeka kwa wimbi hili,Watanzania wawili wamekufa wiki mbili zilizopita baada ya dawa za kulevya walizokuwa wamemeza kupasukia tumboni na kufariki muda mfupi baada ya ndege ya shirika la Ndege la Ethiopia kutua jijini Addis Ababa.
Habari za kuhakiki zinaeleza kuwa dawa hizo zilipasuka tumboni mwa Watanzania hao wakati ndege ikiwa inaendelea na safari zake kwenye anga za juu.
Watu hao waliothibidishwa kupasukiwa na dawa hizo ni Yahya Abdulkadir na Yosuf said,ambao walikamatwa mara baada ya ndege kutua,lakini walifariki dunia baadaye.
Inaelezwa kuwa Watanzania hao walikuwa wakitoka China na kwamba walikuwa wamepanda ndege tofauti za shirika hilo.
Habari kuhusu vifo vya watu hao,zinaeleza kuwa watu hao wakiwa Hospitali dawa kadhaa zilizokuwa bado tumboni mwao ziliendelea kupasuka na kusababisha vifo vyao kwa nyakati tofauti.
Uongozi wa hospitali walikofikishwa Watanzania hao ulieleza kuwa mmoja wao alikutwa akiwa na zaidi ya kete 109 tumboni ambazo baadthi yake zilipasuka.Alifariki wiki mbili zilizopita.
Dk.Behailu Haile,Mkurugenzi wa Hospitali Hayat iliyoko Addis alisema kila kete iliyokutwa tumboni mwa Watanzania hao ilikuwa na uzito wa gramu 15.
Mtanzania mwingine alikufa jumatatu ya wiki hii baada ya kete alizokuwa amemeza kupasuka tumboni.
Madaktari wa hospitali hiyo walisema kuwa Mtanzania huyo aliyefariki jumatatu ya wiki hii alikutwa na kete 42,huku 17 kati ya hizo zilizotolewa baada ya kufariki.
Hadi sasa hakuna habari zozote zilizoeleza iwapo miili ya Watanzania hao imerejeshwa makwao kwa mazishi.
Mkurugenzi wa mashitaka ya makosa ya jinai(DCI),Robert Manumba na Mkuu wa kikosi cha kupambana na Dawa za kulevya,Gedfrey Nzowa,walisema jana kuwa hawana habari na matukio ya Watanzania hao.
Wakubwa hao walisema hawajapokea taarifa zozote kutoka Serikali ya Ethiopia kuhusiana na vifo vya watu hao.
No comments:
Post a Comment