Wednesday, February 18, 2009

Mchungaji Mbeya abambwa na viungo vya albino

POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu wawili wakazi wa Kijiji cha Idweli, Kata ya Iyula, wilayani Mbozi, akiwemo mchungaji wa Kanisa la Pentekoste kwa tuhuma za kupatikana na viungo vya albino ambavyo vilikuwa vikiuzwa kwa Sh 30 milioni.Tukio hilo linalomhusisha mchungaji, limekuja wakati nchi ikiwa katika kampeni ya kupambana na ukatili dhidi ya maalbino, ambayo hupewa msukumo pia na viongozi wa dini mbalimbali.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema mtuhumiwa mwingine ni mkulima wilayani Mbozi.Kamanda huyo alisema kukamatwa kwa watuhumiwa kulikuja wakati wakihaha kusaka wateja katika maeneo ya soko la Mwanjelwa jijini Mbeya.Kwa mujibu wa Kamanda Stephen, watuhumiwa walipofika katika soko hilo Februari 16 , walidai walikuwa wakiuza viungo vya kunguru mweupe. Zelothe alisema kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema, polisi waliweka mtego na kuwanasa baada ya kupatana kuuziana viungo hivyo katika mji wa Mlowo, wilayani Mbozi ambako kachero mmoja alifika Februari 16, kukamilisha mpango huo.Alisema baada ya makubaliano ya kiasi cha Sh 30 milioni kushindikana na kuahidiwa kukamilisha fedha hizo siku inayofuata (Februari 17), kachero huyo alifika na kiasi hicho cha fedha na kupeleka nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa na kukabidhiwa vipande vinne vya viungo hivyo, vikiwemo viganja vilivyohifadhiwa katika magazeti mawili tofauti.Kamanda Stephen alisema baada ya kumkabidhi viungo hivyo, watuhumiwa walikamatwa na walipopekua nyumbani kwa mmoja wao, walikuta dawa aina mbalimbali na maji ya kuchanganyia dawa hizo.

No comments:

Post a Comment