Tuesday, March 24, 2009

MAMBO 18 YANAYOKUFANYA UWE MSWAHILI...


1..Asilimia 90 ya CD pamoja na kanda za cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki AU ni za kuazima.



2.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapokuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k..


3.Mama yako ana migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa miezi 10 au zaidi.


4.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa.

5.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule..

6. Unapenda kuhudhuria / kushiriki hafla na sherehe mbalimbali kama vile harusi, maulidi, Ubarikio n.k ambazo hujaalikwa na wala huhusiki.

7. Unapenda kuomba kununuliwa dola (credit), pombe, soda, sigara n.k

8. Unapoingia katika chombo cha usafiri unapenda kupigania/kukimbilia na hata kuingilia dirishani..

9. Unapohudhuria hafla au sherehe fulani unapenda kubeba bia, maji, soda na chakula kupeleka nyumbani wakati unarudi.

10. Unapenda kutembelea watu ovyo ovyo hata kama hujaitwa au huna jambo la msingi linalokufanya la kukupeleka kwao.

11. Unapenda kuongea saana kuhusu mambo ya watu wengine (Umbea), mara sijui fulani kafanya hivi, mara fulani hana lolote...

12. Unapenda sana kuongea unapokuwa na watu lakini maongezi yenyewe hayana msingi wowote, ili mradi tu uonakane nawe umo.

13. Unapenda sana kusoma magazeti ya udaku, kama vile Kiu, Ijumaa n.k. na pia habari zisizokuwa na elimu ndani yake. Kama vile Baba Ubaya, Toto tundu, Babu suni n.k.

14. Unakuwa mbishi sana kutoa michango ya harusi, ila kwenye mnuso wewe ndio wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka tena ukiwa ndiiiiiii....

15. Unaiga kila kitu toka kwa jirani yako badala ya kubuni mambo yako. Mfano akifungua grocery we nawe unafungua yako ubavuni, akifuga kuku, we nawe umo....

16. Unakuwa huendi out na mkeo na kama mkienda shughulini yeye hutangulia mbele kabisa na wewe unafuata nyuma kwa mbali kama watu baki, na huko mkifika hakuna kujuana. Ukionekana out na mtu basi ni nyumba ndogo

17. Unakuwa kila jambo la kila mtu kazini kwako unalijua, lakini la kwako hakuna anayelijua. ukiulizwa unakuwa mkali kama mbogo

18. Una tabia ya kuandaa pilau na kuku wakati wa sikukuu tu. Halafu mayai, matunda na maziwa unakula ama unaandaliwa ukiwa umelazwa hospitali

No comments:

Post a Comment