Thursday, June 4, 2009


OMBI LA MJADALA

Kuna Watanzania wengi wa jinsia na marika mbali mbali waishio Jijini New York na kwenye vitongoji vyake ambao kwa idadi tungetosha kabisa hata kuunda kamji kadogo, lakini ajabu ni kwamba mpaka wa leo hatujafanikiwa kuunda umoja. Watanzania wenzetu wengi waishio miji mingine na hata nchi mbali mbali duniani kote wamejibiidisha sana katika hili. Nadhani wakati umefika kwa sisi tuishio Jijini hapa kuamka na kutambua ya kwamba "umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu". Tunahitaji kujikusanya na kuunda Umoja wa Watanzania New York, kwa kutambua kwamba tunahitajiana kwenye shida na raha, leo na kesho na hasa hasa ukizingatia kwamba hapa ni ugenini.

Kama mkereketwa nimeonelea nifungue huu mjadala hili nione kama kuna mwenzangu au wenzangu ambao tunalengana kimawazo na kama yuko au wako tayari na hili jambo.
Nawaomba wasomaji wote wa blogu hii mchango wenu katika kuchangia hii mada.

KARIBUNI!!

3 comments:

  1. Asante sana Mr. FUNDI kwa kuwahimiza wana NY kuunda jumuiya ya WATANZANIA.Ni jambo muhimu sana ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka. Tukumbuke kwamba sasa hivi kuna generation ya pili ya Watanzania ambao wanahitaji strong comminity organization ili waelewe walikotoka na wanakoelekea. Generation ya kwanza tumieishaanza kuzeeka na kuingia kipindi stress, maradhi na mengineyo ambayo utatuzi wake mara nyingi unatoka kwenye community husika. Tumeona wenzetu kutoka sehemu mbalimbali ambao hutegemea michango kutoka dunia nzima ili kutatua matatizo yao, sidhani kama NY inahitaji hilo, because we are New Yorkers, we should be the example. Jumuia itatusaidia kutatua matatizo yetu bila mtu kuingiza mkono mfukoni mwake. Kuna mambo fulani ambayo hayaangali kama unafanya kazi WALL-STREET au unadrive YELLOW CAB, mamabo hayo mara nyingi yanahitaji COLLECTIVE EFFORT AS A COMMUNITY.
    SHIME WANA N.Y

    ReplyDelete
  2. Ukabila umezidi sana Newyork. Kuna makabila yanajiona yenyewe bomba sana kuliko wenzao. Kumbuka binadamu wote ni sawa yaani mahitaji yao yanalingana.

    ReplyDelete
  3. Jumuia ni freshi sana ila dharau zimezidi. Wafanya kazi wa UN watakubali kushirikiana na wabeba maboxi? Au wenye pata hadhi duniani (PHD) wataweza kushirikiana na mie wa darasa la saba? Nikishajibiwa nitakubali kujiunga na chama cha Newyork.

    ReplyDelete