Monday, July 27, 2009

MAMBO YA BONGO

Nilipokuwa kwenye likizo yangu niliona mambo/vitu ambavyo vimenifanya nijiulize maswali mengi bila kuwa na majibu.
1. Nilishangazwa sana na jinsi sehemu za starehe(mabaa) wanavyofurika watu katika siku zote za juma(Jumatatu mpaka Jumatatu). Je! hii ina maana ya kwamba uwezo wa watu kifedha ni mkubwa sana au pengine tumegeuka kuwa Taifa la walevi? Au pengine starehe ndio shughuli yetu kubwa na muhimu kuliko kitu kingine. Tukumbuke ya kuwa mtindo huu vile vile unaandamana na mambo mengi yanayochangia kwenye kuiangamiza jamii na kurudisha au kuchelewesha maendeleo ya kweli.

2. Nilishangazwa na jinsi makampuni ya simu yalivyotanda na mabango yao ya matangazo karibu kila sehemu, lakini ni mara chache unaweza ukakutana na mabango ya kutukumbusha kuhusu ukimwi kama vile sio tatizo tena Tanzania.

3. Uongozi wa serikali na chama katika Jiji la Tanga umezorota na unachangia sana katika kukwamisha maendeleo ya Jiji hilo(ambalo hata hadhi ya kuitwa Jiji halina). Waarabu wa Tanga si wapenda maendeleo, na ndugu zangu wa Kidigo itatubidi tuchangamke kama tunataka maendeleo.
4. Wanaoiba si kwamba wanaiibia serikali bali ni sisi sote hivyo tusikubali...

1 comment:

  1. Pointi yako ya kwanza sikubaliani nayo. ukumbuke
    kuna mfanyakazi na mfanya biashara, mfanya biashara anaweza kunywa wakati wowote hiyo ni ela yake mfanyakazi akirudi jioni anaweza naye akanywa wakati wowote ni ela yake.kuhusu matangazo ya ukimwi serekali ndio iwajibike kama unavyojua biashara matangazo hao watu wa simu wanafanya biashara watangaze ukimwi watapata nini?

    ReplyDelete