Monday, September 21, 2009





Usafiri wa baisikeli ni muhinu sana katika hizi nchi zetu za kimasikini. Ukweli ni kwamba zinawarahisishia sana watu katika kufanya shughuli zao bila gharama kubwa. Sioni ni kwanini tusiwe na viwanda zaidi ya kimoja ili kutosheleza mahitaji huko vijijini. Kwa kweli wakati wa likizo yangu Bongo nilikutana na wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu kwenda na kurudi mashuleni na pengine kama kungekuwa na uwezekano wa upatikanaji wa mabaisikeli ya bei nafuu kungepunguza sana hii karaha.




1 comment:

  1. Kule kwetu Usukumani bila baiskeli mambo hayaendi. Nasikia hata kule Tanga mambo ni yale yale.

    Wanafunzi kuendesha mabaiskeli Dar? Sidhani kama ni wazo zuri kwani pengine ni hatari zaidi. Kumbuka madereva huwa hawasimami eti kusubiri mwenye baiskeli apite.

    ReplyDelete