Friday, October 2, 2009



Inakuaje?!Baada ya kupata ajali amesauliwa ! hakuna uduma ya matibabu! wadau tumsaidie Mwanamziki huyu!

Hamisi Kitambi ni mmojawapo wanamziki wakongwe na hadhina waliobakia hapa nchini Tanzania ,bwana Hamisi Kitambi mtunzi wa nyimbo nyingi !mojawapo ya nyimbo zake ni ule wimbo mzuri maarufu kwa jina " Mpenzi wangu !mwenye rangi ya Chungwa" kwa wale wenye kumbukumbu wanajua radha ya utamu wa wimbo huo..

Veteran huyu Hamisi Kitambi amefanya kazi na bendi nyingi zikiwamo Tabora jazz, Unyanyembe band, penginepo KIKO KIDS, labda Dar-es-salam Jazz, labda Western Jazz, hadi anapata hajali ya gari alikuwa Juwata (OTTU) Jazz sasa Msondo Ngoma aka Baba ya Mziki.
Mwanamziki huyu mkongwe Hamisi Kitambi amepata hajali akiwa katika gari yeye na wanamziki wenzie Msondo Ngoma walipokuwa safarini Tanga!
Mzee Hamisi Kitambi kama anavyoonekana pichani,miguu imevunja na amewekewa vyuma, na cha kusikitisha kuwa tangu apate hajali ndio katupwa, hana uduma muhimu. Mtaji wa masikini ni MIGUU YAKE nayo ndio kama anavyoonekana, Je! ni haki kwa mwanamziki au mwanadamu aliyechangia kujenga msingi wa fani ya mziki nchini kutupwa kama hivi?
Basi ata kama hakuna bima ya kulipwa, hata ubinadamu usiwepo?

Tujaribu kumsaidia mzee wetu huyu mwanamziki mkongwe Hamisi Kitambi anapatikana kwa simu hii Dar 0713576475

No comments:

Post a Comment