Wednesday, October 14, 2009

ZIDUMU MILELE FIKRA ZA BABA WA TAIFA!KATIKA KUMKUMBUKA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE, WATANZANIA INATUBIDI KUYAKUMBUKA YALE MAZURI ALIYOYASIMAMIA WAKATI WA UHAI WAKE NA JINSI GANI ALIVYOJITOLEA MUHANGA WAKATI WOTE WA UHAI WAKE KUJENGA MISINGI IMARA WA TAIFA LETU NA WATU WAKE. UMOJA NA AMANI TUNAYOJIVUNIA WATANZANIA HAIKUWA RAISI KAMA SI MWALIMU NYERERE.
WATANZANIA TUKUMBUKE TULIKOTOKA ILI TUJUE TUENDAKO. TUSIKUBALI KABISA KUJENGA TAIFA LITAKAOWAACHA WENGINE NYUMA(TUPINGE MATABAKA), UKABILA, UDINI NA VINGINEVYO VITAKAVYOTUTENGANISHA.

WATANZANIA TUANZISHE VITA KALI DHIDI YA RUSHWA NA UFISADI, NA TUSEME KWA PAMOJA KWAMBA SASA BASI. TUSIWAPE KABISA NAFASI VIONGOZI WENYE SIFA MBAYA KUTUONGOZA TENA NA WATUMISHI WA UMMA WAELEWE KWAMBA WANANCHI NDIO WAAJIRI WAO NA KWAMBA WANA DHAMANA KWETU.

WATANZANIA TUONYESHE KWA VITENDO YALE AMBAYO MWALIMU AMETUACHIA.
MUNGU MBARIKI MWALIMU NYERERE, MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

- Fundi Kombo Ramadhani -