Wednesday, November 11, 2009




Inavyoelekea ni kwamba sehemu kubwa ya elimu yetu haswa ile ya shule za msingi, bado iko nyuma sana. Kuna uwezekano kabisa wa karne ya 22 kutukuta bado tunajiburuza na tuliyoyafanya karne ya 19. Je! hii ina maana ya kwamba hatuelewi umuhimu wa elimu katika maendeleo ya Taifa letu?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba Taifa letu ili liendelee tunaitaji kupambana na vitu vitatu - "Ujinga, Maradhi na Umasikini," na sielewi ni katika mpangilio upi, lakini inaonekana kwamba vyote vinaelekea kutushinda. Siamini kabisa ya kwamba tunawekeza rasilimali zetu kwa kiasi kikubwa katika elimu au tiba na badala yake siku zote tunawarusha watu wetu kwenda nje kwa matibabu na elimu kwa gharama kubwa sana kwa kutumia rasilimali ambazo pengine tungewekeza nyumbani kwa faida ya wengi.
Taifa letu lazima lianze kufikiria kutoa elimu sambamba na ya dunia ya kwanza ni si ya ubabahishaji. Tunahitaji kuinua kiwango cha elimu yetu kwa kuwekeza zaidi kwenye elimu. Ni sawa kabisa kuwa na ma-mall makubwa, lakini je mahospitali ya kisasa tunayo? Au ndio siku zote tutakwenda India na Afrika ya Kusini? Nawaunga mkono watu kama kina Nimrod Mkono kwa kuwekeza kwenye elimu kiuhakika. "Bila kuondoa Ujinga na Maradhi Tanzania siku zote itabaki kuwa Masikini."


-Fundi wa Kombo-

No comments:

Post a Comment