Thursday, December 10, 2009

TUSIJIDANGANYE MIAKA 48 YA UHURU BADO NI
BURE KABISA!!!!

Kama sijakosea ni miaka 48 tokea tupate "Uhuru" na ndoto za wengi bado kutimia. Hivi kweli tuna haja ya kusheherekea kwa chochote? Au ni kaumoja ketu na kutawaliwa na serikali ya CCM kwa miaka hii yote? Au ndio kusema tunaridhika na hali tuliyonayo? Mgao wa umeme, ukosefu wa maji, hali duni ya matibabu, elimu duni, ufisadi uliokithiri, na umasikini ulioshamiri... Watanzania tuamke na kudai zaidi toka kwa hao tuliowaweka madarakani na vile vile tuige kwa wenzetu(kwanini Rwanda wanaweza?). Watanzania mnaokaa mijini msidanganyike na magorofa na maduka makubwa mnayoyaona huko mijini, nendeni vijijini mlikotoka ndio mtaelewa kwamba kumbe bado sana!