Monday, January 11, 2010


UBALOZI WA KUDUMU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, UMOJA WA MATAIFA NEW YORK, UNAPENDA KUWATANGAZIA UMMA WA WATANZANIA PAMOJA NA MARAFIKI ZETU WAISHIO JIJINI NEW YORK, MAREKANI NA VITONGOJI VYAKE KUWA, WAMEFUNGUA KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MZEE WETU MPENDWA HAYATI RASHID MFAUME KAWAWA, ALIYEAGA DUNIA TAREHE 31 DESEMBA, 2009.


KWA WALE WOTE WATAKAOPATA FURSA YA KUFIKA UBALOZINI KWA AJILI YA KUTIA SAINI KITABU HICHO WANAKARIBISHWA. UBALOZI UMETENGA SIKU TATU KWA AJILI HII, AMBAZO NI JUMATATU TAREHE 11 HADI JUMATANO 13 JANUARI 2010, KUANZIA SAA NANE (8) KAMILI MCHANA HADI SAA KUMI NA MOJA (11) JIONI.


KWA VILE MSIBA HUU ULITOKEA KIPINDI AMBACHO UBALOZI ULIKUWA UMEFUNGWA KWA AJILI YA MAPUZIKO MAFUPI, UBALOZI HAUKUWEZA KUWEKA KITABU HICHO MARA BAADA TU YA MSIBA HUU MKUBWA KWA TAIFA LETU KUTOKEA.


ANUANI YA UBALOZI NI HII IFUATAYO HAPA CHINI:

“UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PERMANENT MISSION TO THE UNITED NATIONS,
201 EAST 42ND STREET
SUITE 1700
NEW YORK, NEW YORK 10017”.



NDUGU WATANZANIA, JAMAA NA MARAFIKI- KARIBUNI SANA.


-IMETOLEWA NA UBALOZI WA KUDUMU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA, NEW YORK-

1 comment:

  1. Inabidi maandishi yawe MAKUBWA namna hii???

    ReplyDelete