Monday, April 26, 2010

UDUMU MUUNGANO NA MUNGU UIBARIKI
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Ingawa inakuwa ni rahisi sana kuukosoa au na hata kuutia shaka Muungano wetu, lakini tukumbuke ya kwamba UMOJA wetu ndio nguzo kubwa ya amani na utulivu tulionao. Labda pengine ni kutizama wapi kwenye upungufu ili tuparekebishe na kuimarika zaidi.

Mataifa makubwa na tajiri duniani yanaungana ili yaweze kuimarika zaidi, sasa iweje sisi wanyonge tuwe na mawazo ya kutengana? Tusiyaonee haya matatizo yaliopo ndani ya muungano wetu au kuyafumbia macho. Inatubidi tuyafanyie kazi kwa juhudi ili yasiendelee kutukera mara kwa mara! Wahasisi wa Muungano wetu hawakusema kwamba walimaliza kazi waliyoianza, walijua wazi kwamba jinsi siku zinavyokwenda na dunia inavyozidi kubadilika ni lazima kutaitajika mabadiliko ya  kimsingi ili kuuimarisha muungano.

HERI YA SIKUKUU NJEMA YA MUUNGANO!!