Tuesday, May 18, 2010

Hivi kweli haya ni maendeleo au ni kuiga toka kwa wenzetu?
Kuna hatari ya kuupoteza utamaduni wetu kwa namna moja au nyingine kwani vitu vingi tulivyo na asili navyo vinatutoka taratibu bila ya sisi kujitambua! Vipi ugali na kisavu au makande? Taratibu kila kona ya miji yetu itakuwa imetawaliwa na migahawa ya kigeni... na hayo ndio maendeleo!!
Inavyotokea kwenye lugha zetu za kikabila ndivyo hata vyakula vyetu asilia vitakavyopotea. Katika miji yetu mingi vijana wengi walio kati ya umri wa miaka 18 mpaka 30, lugha za wazazi wao hazipandi tena. Tanzania tuna makabila 120 au zaidi sasa iweje asilimia kubwa ishindwe kuzungumza kwa kutumia lugha asilia?

No comments:

Post a Comment