Friday, May 21, 2010

Sio lazima uwe na akili nyingi kuelewa kuwa tatizo la fujo na misongamano mijini mwetu(Bongo), inatokana na tulivyoruhusu kiholela vijibasi(Daladala) kutawala mabarabara ya miji yetu kana kwamba ndio vimekuwa mkombozi wa tatizo la usafiri. Nakumbuka wakati tulipokuwa na UDA pale Dar enzi hizo, angalau hali  ilikuwa inafanana fanana na picha za hapo juu. Kulikuwa na kaustaarabu ka aina fulani. Labda pengine, tufikirie tena kuwa na mashirika kama UDA na tuondokane kabisa na hili balaa!