Thursday, July 1, 2010

Duku duku la uchaguzi wa mwaka huu limekwisha anza kwa wagombea kuanza kuwakilisha fomu zao akiwemo pia Mheshimiwa raisi kwa tiketi ya CCM(Chama Cha Mapinduzi).

Swali moja linalopaswa kujibiwa, ni nini haswa maana ya uchaguzi wa 2010 kwa Mtanzania na Tanzania? Swali hili linatupasa kukitazama upya chama cha "MAPINDUZI" na kuona kama kweli kinaweza kujigeuza na Kuwa 'CHAMA CHA MAENDELEO". Labda pengine bado kuna mgongano wa kiitikadi tokea wakati kuanzishwa kwake hadi sasa hivi. Lugha ya sasa hivi si mapinduzi bali ni maendeleo na hayawezi kuja kwa mkakati tuliouweka mwaka 1977.

Dhamana ya nchi yetu bado iko mikononi mwa CCM, na kama uongozi wa chama hautaona umuhimu wa kubadilisha mwelekeo wake, basi tujue wazi kwamba mambo yatakuwa ni yale yale! Chama kinahitaji uongozi wenye fikra mpya na tofauti and some people should step down...