Sunday, July 11, 2010

Spain

Netherlands

Yakiwa yamesalia masaa machache kuanzia sasa, karibu wapenzi wote wa soka Duniani wataelekeza macho na masikio yao kule Afrika ya Kusini ili tu kutaka kushuhudia ni nani atakuwa bingwa wa kandanda Duniani 2010 kati ya Spain na Netherlands. Utabiri wa blogu hii hapo awali uliipa Spain ubingwa....

Afrika ya Kusini inastahili pongezi za dhati kwa yale yote waliyoweza kuyafanya kuhakikisha kila aina ya mafanikio kwa mashindano haya makubwa duniani, kinyume cha wengi ambao walidhani kutatokea kila aina ya mushkeli kama vile kuchelewa kwa ujenzi, ualifu, fujo na mengi mengineyo.
HONGERA AFRIKA YA KUSINI, HONGERA AFRIKA!!!!!