Sunday, August 29, 2010

MAO NA SOPHIA WAMEREMETA!!

Siku ya Ijumaa na Jumamosi tarehe 27th na 28th August, 2010 ilikuwa ni patamshika katika jiji la New York hususan pale Mt. Vernon na New Rochelle wakati ndugu zetu Mao na Sophia walipotujumuisha katika harusi kabambe ya Mwaka 2010.

 HONGERA SANA MAHARUSI!!!


 
Maharusi wakiwa wanaingia ukumbini kwa madaha ya hali ya juu!


Maharusi wakijitayarisha kukata keki!!


Dj wetu maarufu toka Minnesota ambaye hata haitaji hutambulishi alikuwepo kuwarusha watu kwa siku zote mbili za sherehe!


Palikuwa hapatoshi....


Wadau mbali mbali waliwakilisha!

Kulikuwa na baa katika kila kona ya ukumbi na kila aina ya kinywaji!


Nikila mapozi na wanaosadikiwa kuwa waanzilishi wa jumuhiya ya Wabongo New York,  Bwana Fredrick Chagula na Bwana Henry Stambuli


Tukijitayarisha kuingia ukumbini na mama!!


Wakina dada wakila maraha usiku wa mkesha wa harusi!


Mdau wa Boston, Innocent naye alikuwepo kuwakilisha mkeshani.


Bwana harusi alionekana kuwa mtulivu na tayari kwa harusi usiku wa mkesha.

No comments:

Post a Comment