Thursday, August 19, 2010

Mziki wa Ngoma Africa Band wapokelewa kwa NGUVU na KASI Kubwa Zaidi na washabiki

FFU wa Ngoma Africa Band wakitingisha jukwaa la World Music Festival,Mjini Loshasen,ujerumani ambapo mziki wao ulikubalika na washabiki na kuweka rekodi ya kuwa bendi bora iliyoweza kuwanasa washabiki na kupelekana na puta bila mapunziko.

Bendi hiyo yenye tabia za kuwadatisha hakili washabiki na mdundo wao "Bongo Dansi" imejiozolea umarufu kila kona duniani na kufanikiwa kujizolea mihaliko ya kutumbuiza katika majukwaa mbali mbali,kutokana na tabia zao hizo za kuwadatisha hakili washabiki kwa njia ya mziki "Ngoma Africa band" imejikuta bize bila ya kumpuzika kwa kuwatumikia washabiki na kuwapa mziki ambao unahitajika kwao!

hata hivyo gwaride la FFU litaendelea kupiga kasi kwa nguvu katika jukwaa la ALAFIA Festival mjini Hamburg,ujerumani siku ya 29.08.2010

onyesho litafanyika katikati ya kitovu cha mji wa Hamburg,Hamburg-Altona.

Pata raha zaidi at www.myspace.com/thengomaafrica

No comments:

Post a Comment