Friday, October 8, 2010

CHAMA CHA JUMUIYA YA WA-TANZANIA NEW YORK.

Well kwa wananchi tunaoishi jijini New York na vitongoji vyake kama New Jersey, na Connecticut tunapenda kuwakaribisha sana kujiunga na chama kipya ambacho kipo njiani kupatiwa usajili. Ni chama ambacho kipo wazi kwa wa-Tanzania wote bila kujali dini, kabila wala rangi au location. I understand kwamba tumekuwepo hapa mjini kwa muda mrefu sana bila ya chama kinachoeleweka na kukubalika na wengi, yaani sisi wananchi. Sasa ninaamini wakati ni huu sasa tukawa na chama kinachowajumuisha wananchi wote wa mjini hapa na vitongoji vyake. Chama tayari kina viongozi wa muda na kinatayarisha uchaguzi mkuu wa viongozi wake wa kudumu, utakaofanyika February, mwakani 2011 kwa tarehe itakayosemwa baadaye, kwa maelezo zaidi unaweza kupitia: info@nycmetro.org au Jumuiya ya wa-Tanzania NY @Facebook.

Naibu Katibu Mkuu (Interim).


William Malecela.

No comments:

Post a Comment