Monday, October 25, 2010


Ni jukumu letu kuwajengea mazingira mazuri hawa watoto wetu kwani wao ndio Taifa la kesho! Tazama jinsi wengi wao wanavyokwenda mashuleni bila hata viatu na hata wafikapo mashuleni inabidi wasaidie kuchota maji na madarasani wanakaa wamebanana.  Mimi nakataa kuamini kabisa ya kwamba katika miaka karibu 50 ya kujipatia uhuru, haya yote hatuyaoni...  Elimu na huduma za Afya ni wazi kabisa ya kwamba hazijapewa kipaumbele.  Ujengaji wa mashule katika kila kata sio jawabu! Kuna tofauti kubwa kati ya "Quantity na Quality".   Tukiendelea kupuuzia elimu basi tujue wazi kwamba taifa litadidimia!!!

No comments:

Post a Comment