Tuesday, January 11, 2011


Bendi maarufu ya mziki wa dansi "Ngoma Africa band" aka FFU yenye makao yake nchini ujerumani, Imeuhakikishia ulimwengu kwa mara nyingine kuwa "Bongo dansi" kutoka bongo tambarale ni fyagio la
kimataifa.Baada ya bendi hiyo na "Mzimu wake wa dansi" kutingisha jukwaa la maoenesho ya kimataifa
ya "Kunstendorf Film and music festival" yaliofanyika nchini Serbia kuanzia januari 5 hadi 10.

Kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja aka kamanda wa FFU,alikiongoza kikosi chake jukwaani siku 7 januari 2011 majira ya saa 6.00 usiku na kuanza kuungurumisha mdundo wa "Bongo Dance",ilichukua takribani dakika chache tu mziki huo kutua katika masikio ya washabiki na hapo ndipo palipoanza kulipuka mshike mshike wa nguo kuchanika! washabiki walijikuta wamepagawa akili,na kujimwaga uwanjani.baadhi ya watu walio udhuria walikuwemo viongozi wa ngazi za juu wa serbia,nao walijukuta wameachia viti vya VIP na kujikuta wamejinganya kisawa sawa!walinzi wa vigogo hao walijikuta wana kazi kubwa ya ziada!

Onyesho hilo lilikuwa likirushwa hewani moja kwa moja na TV za
Poland,Serbia,Montenegro,St.Petersburg,Bosnia,Croatia,pia TV hizo zilimuhoji Ras makunja,ambaye alikubali mihaliko mingine ya kutumbuiza nchini Poland,Serbia,Bosnia,Croatia na St.Petersburg,Urusi.

Vianzo vya habari vya nchi hizo zimemtaja Ras Makunja na mzimu wake Ngoma Africa band,kuwa mziki wao ni mdundo wa aina yake na unachezeka,CD za bendi hiyo zimeshaanza kupigwa katika vituo vya redio za nchi hizo.

Katika maonyesho hayo wanamziki wa ngoma africa band walikuwa wakilimudu jukwaa na kushambulia kama vile hawana akili nzuri,mpiga solo Chris-B aka "Mshenzi" alikuwa akifinya solo gitaa lake...na uku dansa wa ffu Dada Bedi La Bella Bella akienda sambamba na Ras Makunja kuhakikisha kuwa washabiki wanatolewa Knock Out.

Ras Makunja na bendi yake imekuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumbuiza nchini humo toka vita vimalizike,na washabiki wameukubali mziki wa Bongo Dance kutoka Bongo Tambarale kuwa ni moto wa nyikani.....

wasikilize ffu at www.reverbnation.com/ngomaafricaband



No comments:

Post a Comment