Thursday, February 17, 2011

"INASADIKIWA KUWA ZAIDI YA WATU 20 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE 145 KUJERUHIWA"
Ndani ya kipindi cha miaka miwili tunashuhudia maafa ambayo yamesababisha watu wengi kufariki na wengine wengi kuumia na hasara kubwa kutokana na mali nyingi kuteketezwa. Je! tumejifunza nini kutokana na maafa haya? Uwezekano wa kutokea tena ni mkubwa sana kama hatua za taadhari hazitachukuliwa. Mojawapo ya hatua muhimu ni kuyasogeza mbali zaidi haya maghala ya silaha mbali na maeneo wanamoishi raia.
"MATEGEMEO NI KWAMBA JESHI AU SERIKALI ITAWAFIDIA WALIOKUMBWA NA MAAFA HAYA"