Tuesday, March 8, 2011

UTUMWA!!!

Ni vizuri kwa kizazi cha sasa kikafahamu kwamba mpaka kufikia hapa tulipo, mababu na mabibi zetu walifehedheshwa na kukatiliwa sana na wageni waliovamia nchi zetu na kutufanya nusu wanyama. Hali hii bado haijesha na kama watapata nafasi tena bado watataka kututawala lakini kwa namna tofauti kabisa.

Machochezi tunayoyaona ya vurugu za wenyewe kwa wenyewe ni mojawapo tu ya njia hiyo ya kutaka kututawala kwa kuwatumia vibaraka ambao ni wenzetu kabisa.  Ukoloni bado upo na hawa Wakoloni wanaitamani sana Afrika yetu kutokana na wingi wa rasilimali zake, kama vile mafuta, madini, wanyama pori n.k. Afrika inahitaji viongozi wasioyumbishwa na wenye mwelekeo.

Inastahajabisha sana kuona mpaka wa leo nchi nyingi za Afrika bado zina matatizo makubwa ya umeme, maji na chakula na bado hakuna ufumbuzi wa kweli wa matatizo haya.  Hawa wakoloni wanaodai kuwa  ni marafiki zetu na wako tayari kutusaidia kuleta maendeleo kwa kubadilishana na mafuta na madini yetu, kwa nini basi wasituondolee haya matatizo ya umeme, maji na chakula ili nasi tuwe kama wao? 

China, Ulaya, Marekani na wengine wote bado nia yao ni ile ile!!