Tuesday, May 17, 2011

FFU wa Ngoma Africa Band jukwaani tena! 28-05-2011 mjini Burg satzvey jirani na BONN, Ujerumani

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye maskani yake nchini ujerumani, inatazamiwa kutumbuiza katika maonesho ya  Afrika & Orient Festival,huko mjini Burg Satzvey jirani na miji ya Bonn na Koln,nchini Ujerumani,siku ya jumamosi 28.Mai.2011 kuanzia saa 1.00 usiku.


Kamanda wa kikosi kazi hiko Ras Makunja wa FFU atakiongoza jukwaani kikosi machachari na kuhakikisha kuwa gwaride la mziki linamfikia kila mshabiki.. Bendi hiyo yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji wakiwemo wacharaza magitaa wakali kama vile Chris-B,Said Jazbo Vuai,Maxime buanda..na wengineo,Ngoma Africa band pia maarufu kwa tabia  yao ya kuwadatisha akili na kuwatia kiwewe washabiki.


Bendi hiyo imetajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyofanikiwa kuufanya muziki ndio daraja na urimbo wa kuwanasa mamilioni ya wasahabiki katika kila kona duniani...


Ngoma Africa band ilianzishwa mwaka 1993 pia imetajwa na vianzo vingi vya habari kuwa ni bendi pekee ya kiafrika iliyoweza kuimiri vishindo vingi vya washabiki sugu barani ulaya..na kila wanapotumbuiza katika maonyesho ya kimataifa  wanakuwa na kazi moja tu... nayo ni kuhakikisha washabiki wanapagawa na kudata akili...


wasikilize zaidi


at www.reverbnation.com/ngomaafricaband  au www.myspace.com/thengomaafrica


No comments:

Post a Comment