Thursday, August 25, 2011

JINAMIZI LA MUZIKI WA DANSI BADO LINAFUNIKA ULAYA !

Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni!
Kuvaana na washabiki Mjini Tuttlingen,Jumamosi 27.08.2011


Bendi maarufu ya mziki wa da nsi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini ujerumani inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa la Afrika Festival,mjini Tuttlingen,huko Ujerumani ya kusini.

Kamanda Ras Makunja atakiongoza kikosi chake jukwaani siku ya jumamosi 27.08.2011,bendi hiyo imetajwa ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya yenye mafanikio ya kuwanasa washabiki wa kimataifa kwa wingi,pia kutumia muziki wake made in bongo uswahilini kama daraja au urimbo wa kuwanasana washabiki katika kila kona duniani,na kuwapa burudani ya aina yake.

Wakali hawa wa mziki wa dansi kwa sasa wanatamba na nyimbo zao mbili mpya "Bongo Tambarare " na "Supu ya mawe" wasikilize zaidi at www.ngoma-africa.com
tafadhali usisahau ku log in at www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment