Monday, August 8, 2011

Washabiki wa Frankfurt walivamia jukwaa la FFU wa Ngoma Africa band,
kamanda wa FFU Ras Makunja katika kazi ya ziada !




 
Ilikua jumamosi ya asiye na mwana abebe jiwe ! katika tamasha la Afro-karibik, Robstock park,Frankfurt,ujerumani. Pata shika la nguo kuchaika kati ya ffu wa ngoma africa band na washabiki sugu mjini Frankfurt, katika onyesho ambalo washabiki walionyesha ubabe dhidi ya walinzi na kulikwea jukwaa baada ya kudatatishwa na mdundo wa Ngoma Africa band aka FFU.
 
Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja alikiongoza jukwaani kikosi chake ambacho mshambuliaji wa gitaa la solo Chris-B aka "Mshenzi" wa gitaa,alikua akipereka makombora mazito ya milio ya nyuki katika gitaa. Safu ya washambuliaji wa mbele ikiongozwa na kamanda ras makunja, akiwemo Diva Princess Bedi Beraca bella, ilikua na kazi ya moja tu.. nayo kushambuliana jino kwa jino na washabiki.
 
Washabiki nao walipopandisha mzuka wao wa mziki walirudisha mashambulizi ndani ya ulingo wa dansi ! si watoto wala wakubwa,wanawake kwa wanaume! wazungu na weusi wote wamedata akili mbele ya mziki wa ngoma africa band aka FFU,onyesho la jumamosi 6.08.2011 kule frankfurt Ujerumani.
wasikilize zaidi FFU at www.ngoma-africa.com

1 comment:

  1. Ngoma Africa band aka ffu,aka watoto wa mbwa,muziki wenu unakubalika,vipi ?kuna mpango wowote wa tour ya U.S ?

    ReplyDelete