Friday, November 4, 2011

Ngoma Africa Band na Nyimbo mpya za miaka 50 ya Uhuru,


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU,yanye makao yake nchini
Ujerumani,wameachia hewani CD mpya yenye nyimbo za miaka 50  ya Uhuru. Nyimbo zilizomo katika CD hiyo ni utunzi na uimbaji wake kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na Chris-B,mpiga solo wa kikosi hiko,habari za uhakika zimetonya kuwa nyimbo hizo zimetua pia katika blog mashuuriya Michuzi,pia vituo vya Redio vya Deutche Welle mjini Bonn,Radio VOA ya Washington, Radio Free Africa, Mwanza, vimepoke nyimbo hizo ambazo wakati wowote zinaweza  kutoa burudani kwa wananchi katika shamra shamra za miaka 50 ya uhuru.
Nyimbo hizo mbili (1) Miaka 50 Uhuru(rumba) na 2. 50 Uhuru Shangwe, Zinasikia pia at www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment