FFU wa NGOMA AFRICA
BAND WAMESHATUA BERLIN!
Kwa kutumbuiza katika Sherehe za miaka 50 ya Uhuru
Ijumaa 9 na Jumamosi 10 Dec 2011 Berlin
Hapatoshi FFU wa Ngoma Africa Band
kutoa burudani ya kukata na Mundu, CD ya "50 Uhuru
Anniversary" inatamba Redioni
Watanzania wanaoishi Ujerumani
! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru !
Berlin Chereko !Chereko
! Umoja wa Tanzania Ujerumani
(UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!
Kikosi Kazi cha Ngoma Africa band aka FFU,kimeshatua mjini Berlin kwa kazi
moja tu, nayo ni kushambulia na muziki wake katika kusherekea miaka 50 ya uhuru wa
Tanzania.
Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011
mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio mji mkuu wa
Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi wa UMOJA WA WATANZANIA
UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja huo unawaunganisha watanzania
wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na
viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na Bi.Tullalumba Mloge
(katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9
mchana hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na
muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin,
UMOJA NI NGUVU WATANZANIA
JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU !
sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment