Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindi viti mbalimbali ikiwemo ubunge wa Arumeru Mashariki, Chama tawala CCM kimekubali kushindwa na kuipongeza CHADEMA.
katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amesema “tunawapongeza kwa ushindi walioupata, tunakipongeza chama kama chama pia, tumempongeza Nassari lakini tukatoa wito ikiwa yeye kama kijana ajitahidi kusukuma kwa kuhakikisha yale aliyoahidi yanatekelezeka ili watanzania waendelee kuwaamini vijana, sisi kama Chama tumepokea kwamba tumefanya kampeni kwa siku zote lakini wananchi wa Arumeru wamewachagua wao na sisi tumelipokea kwa mikono miwili kwamba ndio sauti ya wana Arumeru”
Nnauye ameamplfy zaidi kwamba “tumekubaliana na matokeo na ndio maana tumechukua hatua ya kuwapongeza, sasa maneno mengine yooooote yatakayosemwa ni maoni ya watu lakini msimamo wa chama chetu ni kwamba tunataka tuue dhana ya kwamba uchaguzi ambao ni huru na haki ni ule ambao wewe umeshinda, usiposhinda basi haukua huru na wa haki, sisi hatuamini katika hilo….. la pili tunaamini katika asiekubali kushinda sio mshindani kwa hiyo sisi tumekubali, inawezekana tuliteleza mahali au mbinu za mikakati uwanjani walituzidi wenzetu ndio maana wameshinda, tumekubali na tunawatakia kila la kheri” |
No comments:
Post a Comment