Tuesday, April 3, 2012

KABLA YA KUSHINDA UCHAGUZI WABUNGE WA CHADEMA WAPOKEA KICHAPO MWANZA.


Wabunge wa CHADEMA Mh. Highness Samson Kiwia (Ilemela) kushoto na Salvatory Machemli (Ukerewe) wakivuja damu baada ya kuvamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana.

Mh. Highness Samson Kiwia mbunge wa Chadema Ilemela akionesha jiraha alilopata mgongoni kwa kukwatwa na panga.


Majeraha ya kichwani ya mbunge wa Chadema Ilemela Mh Higness Kiwia baada ya kukatwa mapanga na watu wasiojulikana

Mh. Highness Kiwia mbunge wa Chadema jimbo la Ilemela Mwanza akielezea tukio baada ya kupata ichapo toka kwa watu wasiojulikana huko Mwanza.


Wabunge wawili wa Chadema wamejeruhiwa vibaya kwa mapanga na mashoka jijini Mwanza katika tukio lililotokea saa nane usiku katika eneo la Ibanda Kabuhoro baada ya kuvamiwa na watu ambao bado haijajulikana walikuwa na dhamira gani katika usiku wa kuamkia uchaguzi wa diwani Kata ya Kirumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow alisema jana kwamba mbali na wabunge hao, Samson Highness Kiwia wa Ilemela (kushoto) na Salvatory Machemuli wa Ukerewe (kulia) PICHANI, wengine walioshambuliwa ni pamoja na Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada wa UVCCM aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia.

Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.
Awali, wabunge hao walilazwa katika Hospitali ya Rafaa Bugando lakini baadaye walisafirishwa kwa ndege kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. Kwa upande wake, Waziri amelazwa Bugando.

Kamanda Barlow alisema katika vurugu hizo magari matatu likiwemo la Kiwia yaliharibiwa.
Polisi ilipata mapema taarifa za tukio hilo lakini ilichelewa kufika kutokana na eneo hilo kuwa lenye mawe na milima hivyo kufika wakati tayari wabunge wameshajeruhiwa vibaya na mali hizo kuharibiwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mabina amekana wafuasi wake kuhusika na uvamizi huo dhidi ya wabunge hao, akidai kwamba pengine wabunge hao walikutana na wahuni au majangili wakawavamia na kuwashambulia kwani mazingira ya usiku namna hiyo huwezi kuamini kwamba CCM wamefanya shambulio hilo nakuwataka wabunge hao wahojiwe zaidi walikwenda kufanya nini maeneo hayo nyakati hizo. 
  

No comments:

Post a Comment