Mama mzazi wa Marehemu Steven
Kanumba, Flora Mtagoa. MAMA mzazi wa Marehemu Steven
Kanumba, Flora Mtagoa amemzungumzia msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’
anayetuhumiwa kuwa ndiye chanzo cha kifo cha mwanaye na kusema yeye
hawezi kumchukia kwani anaamini kilichotokea ni mipango ya Mungu. Akipiga
story na Ijumaa nyumbani kwa marehemu, Vatican Sinza alisema kuwa yeye
kwanza hamjui Lulu na wala hajawahi kukutana naye, wala hakuwahi kujua
kuwa ana uhusiano na mwanaye kwa sababu hakuwahi kupewa utambulisho. “Namshukuru
Mungu ingawa inauma na ni vigumu kuamini lakini siwezi kumlaumu wala
kumchukia mtu, ninachoamini Mungu amempenda zaidi mwanangu na amekufa
kama wanavyokufa wengine,” alisema mama huyo kwa masikitiko. |
No comments:
Post a Comment