WAZEE wa Klabu ya Yanga wamezidi
kuitibuka baada ya leo baraza la wazee wa klabu hiyo kutangaza kuwepo
kwa mvua ya masika klabuni hapo iwapo mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd
Nchunga na wajumbe wake wa kamati ya utendaji hawatojiuzulu kwa hiyari
yao kabla ya kufikia Mei 20 mwaka huu.
Wazee hao wamemtaka makamu mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo, Ridhwan Kikwete kusikia machungu
kama waliyonayo kwani ni yeye aliyechangia kumleta madarakani Nchunga,
“Ridhawan mbona hulii kama wazee wako wewe ulitushawishi kumchangua
Nchunga? alihoji Katibu wa baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali.
Akizun gumza na
waandishi wa habari jana makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na
Twiga, Akilimali alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na uongozi wea
Nchunga kushindwa kuongoza na hivyo kuisababishia matatizo mbalimbali.
Alisema kuwa wameunga
mkono maamuzi aliyoyatoa Nchunga ya kutaka kuzungumza nao Mei 20,
lakini wanashangazwa na taarifa hizo kwa kuwa aliwakana na kusema katiba
ya Yanga haina wazee, hivyo wao wameona siku hiyo iwe ni kwa ajili ya
mkutano mkuu wa wanachama wote, huku akiwaomba wanachama kujitokeza kwa
wingi ili kushuhudia Nchunga akijiuzulu. Akilimali alisema kwa mjumbe
yoyote wa kamati ya utendaji atakayejiuzulu kabla ya siku hiyo
watammthamini, lakini kwa yule atakayeendelea kutaka kubaki madarakani
watamuondoa kwa nguvu.
“Nchunga alituambia sisi waongo kusema wachezaji wanadai pesa
wakati tunatambua kuwa walipoewa shilingi 300,000 ili kuwatuliza na wale
ambao anawaita wauza unga. “Wanayanga na Watanzania mmewasikia
wachezaji wakilia njaa sijui nani ni muongo kati yetu, Sisi tulitaka
timu kwa maslahi ya Yanga na si vinginevyo,”aliongeza Akilimali “Nchunga
kwa maslahi ya Yanga ni vema akaachia ngazi kwani Yanga ikiendelea kuwa
chini hapatatawalika waswahili tunasema ''Ukiona Manyoya ujue Kaliwa'',”aliongeza Akilimali ambaye aliungwa
mkono na wazee mbalimbali wa baraza hilo wakiwemo Yusuf Mzimba, Bilali
Chakupewqa, Jabir Katundu na wengine.
Akienda mabli zaidi,
Akilimili alisema baraza hilo limekusanya kiasi cha mil.750 ambazo
watazitumia kwa ajili ya kulipa madeni ya wachezaji na wafanyakazi wa
Yanga,pamoja na kuzitumia kwa ajili ya usajili wa wachezaji wa ndani na
nje ya nchi, pia kutafuta kocha mpya atakayeinoa timu hiyo baada ya
Kostadin Papic kumaliza muda wake.
Aidha, wazee hao
waliwata wanachama wote wa Yanga kutolipa ada ya uanachama ya sh.12,000
kama walivyotakiwa na Nchunga ili kushiriki mkutano huo, pia mjumbe wa
bodi ya udhamini Yusuf Manji kuacha kutoa mil.12 kila mwezi na shilingi
mil.75 ambazo amekuwa akitoa kwa ajili ya kuendesha klabu, kusitisha
zoezi hilo mpaka watakapotangaziwa.
“Kama Nchunga
hatokubali ombi letu hili kwa madai ya kutokuwa na fedha za kugharamia
mkutano siku hiyo aseme ili tushughulike sisi kwa kila kitu kuanzia
kutafuta ukumbi na kulipia, usafiri, chakula na mengine kwa ajili ya
wanachama toka sehemu mbalimbali nchini ambao watakuwa tayari
kushiriki,”aliongeza.
Aliongeza kuwa
anashangaa klabu hiyo kuwa na hali ngumu ya kiifedha wakati mwenyekiti
aliyepita Iman Madega aliacha benki sh.mil.200, kampouni ya Bia Tanzania
(TBL) inatoa mi.17 kila mwezi, kadhaliki Manji anayetoa Mil.75 pia kila
mwezi lakili fedha zote hizo hazijulikani zinapokwenda.
|
No comments:
Post a Comment