Tuesday, May 8, 2012

HIZI NDIO DILI MBILI ALIZOZIPATA MWANAMITINDO FLAVIANA MATATA TOKA MWAKA UANZE.

Hii nafasi inamilikiwa na mbongo ambae anashika nafasi ya pili kwa kuwa na followers wengi kwenye twitter, akiwa na zaidi ya watu elfu 27, 500.
Ni Miss Universe wa zamani wa Tanzania, model wa kimataifa aliesain na Next Models pamoja na Boss, mtoto wa kitanzania mwanamitindo Flaviana Matata.
Huu ukiwa ni mwezi wa tano toka 2012 ianze, tayari Flaviana ameweza kupata nafasi ya kufika sehemu ambayo ni wanamitindo wachache sana wa Afrika wanaweza kufika.
Tayari kwa mwaka huu pekee Flaviana amepata dili mbili kubwa za New Look Campaign na Kenzo Campaign.
Akisikika kutoka London ndani ya AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Flaviana amesema “nimefanya vitu sio vingi sana mwaka huu, nimerudi kazini january mwishoni nimefanya fashion week nimemaliza, nimepata campaign za Kenzo na New Look ambapo ya New Look tayari iko kwenye store sasa hivi around Europe manake wana maduka Eurepe tu na Dubai, pia Editorials kwa different magazines na Catalog shoots kwa designers mbalimbali”
Flaviana ambae makazi yake kwa sasa ni London U.K  na New York Marekani ameamplfy zaidi kwamba ” Kenzo campaign ni maarufu na kubwa sana duniani na kila model anataka kuifanya japo ni wachache sana wanaofanikiwa, industry ni ngumu sana Millard, ni ngumu kumuona model mweuzi akifanya kazi na tuko wengi sana ndio maana pale unapopata kazi lazima upige goti.. “
Amesema “Kama new Look tumefanya models sita lakini wameweka mwafrika mmoja kwa hiyo nafasi kwa weusi ni chache sana hauwezi kwenda kwenye show ukute waafrika nane wazungu wawili, No…. kikawaida utakuta wazungu nane na mwaafrika mmoja au wawili, nahisi wanaweka waafrika wachache tu ili wasionekane wabaguzi lakini yote kwa yote ubaguzi bado upo hatupati nafasi kama wanazozipata wenzetu na sio kwamba tuko wengi kama walivyowao”

No comments:

Post a Comment