ALICHOSEMA WAZIRI MKUU KUHUSU KUCHUKULIWA HATUA KWA WATAKAOONEKANA WANAKULA MCHANA ZANZIBAR KIPINDI HIKI CHA RAMADHANI.
Stori kutoka kwenye bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania July 26 2012 ni kuhusu Swali alilouliza
Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Swali la Mchungaji lilitokana
na taarifa kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa tamko
kuwachukulia hatua wananchi watakaoonekana wanakula mchana au kuvaa nguo
fupi wakati wa mfungo wa Ramadhani.
Mch Msigwa alimuuliza Waziri
mkuu “Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nimesema haina dini,
je ni wakati muafaka kwa Serikali yako kutangaza sasa kwamba upande
mmoja wa Muungano una fuata sheria za kidini na upande mwingine wa
Muungano hauna dini?
Kauli aliyoitoa Waziri mkuu
kumjibu mchungaji Msigwa ni hii…. “Nasema hili kwa maana ya mazingira
ya Zanzibar, ukienda Zanzibar tungechukua tu takwimu za jumla jumla
unaweza ukaona kabisa karibu asilimia 99 hivi ni Waislamu, sasa ndio
maana nasema kwa mazingira ya Zanzibar viko vitu ambavyo vinaweza
vikafanyika na mimi nadhani kwa sehemu kubwa atakua alipima vilevile
mazingira, usilifanye likawa jambo kuuuubwa, angekua anazungumza kwamba
serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ofcourse ingekua tofauti”
No comments:
Post a Comment