MKUU
wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula akiangalia miili ya Marehemu
waliokufa katika ajali ya Gari jana Wilayani Geita,miili hiyo ilikuwa
imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya
hiyo.
NA DAVID AZARIA
WATU
11 wamefariki Dunia Papo hapo hapo na wengine 12 wakijeruhiwa vibaya
baada ya magari matatu mawili kati yao yakiwa ni ya abiria waliyokuwa
wakisafiria kupata ajali na kupinduka wilayani Geita Mkoani Geita.
Tukio
hilo limetokea jana Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha
Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi
la Bunda na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.
Katika
tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku
wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini
huku mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika
chumba cha Upasuaji.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia gazeti
hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a
kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari
yaliyopata ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota
Corola,na T 421 BHS Toyota land Cruiser.
Aliwataja
waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante (18) mkazi
wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani mjini
Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo
(36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote
wakazi wa Kalangalala mjini Geita.
Alisema
bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado
hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11
waliofariki wametambuliwa na ndugu zao.
Kamanda
Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na kulazwa
katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao
ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando
kwa matibabu zaidi.
Mganga
mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza madaktari
wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili
aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji
hospitalini hapo.
Akisimulia
tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni mwendo
kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la
‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land
Cruiser.
Kamanda
Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka mjini
Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo
baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla
likakutana na gari linguine mbele.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili
ya marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.
Akizungumza
na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya jingo hilo
la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa Mkoa
alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa
maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.
Habari kwa hisani ya blog ya GEITA YETU
No comments:
Post a Comment